Makala hii ya mafunzo inachunguza upatikanaji wa teknolojia za kilimo kwa wanawake katika kanda tatu za Tanzania ambazo ni Arusha, Morogoro na Mtwara. Mradi wa SSBVC ulitekeleza shughuli ya Evoucher ambayo hutoa vocha za kieletroniki kwa wajasiriamali wadogo (SE) kupokea vifaa vya kilimo kwa punguzo la bei ili kuboresha uzalishaji. Dhumuni la mfumo huu wa punguzo la bei kupitia E-voucher ni kuchochea muingiliano baina ya washirika katika soko na kusisimua ugavi na mahitaji . Mfumo huu kimkakati unakuza mabadiliko endelevu kwakuwa punguzo la bei huwalenga wale wenye uhitaji zaidi huku ukionesha manufaa ya kuimarisha vifaa vya kilimo na kuwezesha matokeo ya mafunzo kwa vitendo ili kutengeneza mahitaji kwa wajasiriamali wengine waweze kutumia vifaa hivyo. Ili kujua idadi ya wajasiriamali wadogo (SE) waliofikiwa kupitia shughuli hii ya E-voucher, mradi ulilenga kujua wanunuzi wa vifaa hivyo vya kilimo na kuchanganua waliofadika na shughuli hii. Hata hivyo, utafiti huu uliingia ndani zaidi ili kuweza kujua “ haki kwenye mali (samani)” ambapo ilijumuisha manunuzi lakini pia matumizi, umiliki na udhibiti.