Sep 14, 2021 | by MEDA
Tangu 1953, MEDA imekuwa ikiandaa na kutekeleza mipango inayozingatia soko na hivyo kusaidia mamilioni ya watu kote ulimwenguni katika kufikia matarajio yao ya kiuchumi na kijamii. MEDA inaunganisha suluhisho bunifu za sekta binafsi na kujitolea kwa maendeleo ya jamii zilizotengwa kimfumo, zenye kipato cha chini na duni. Kama mbunifu kiufundi anayebadilika, utaalamu wa MEDA ni pamoja na mifumo ya soko, minyororo ya thamani, desturi za kilimo zinazostahimili tabia nchi na endelevu kimazingira, huduma za kifedha, na uwekezaji. Miradi yetu inazingatia ujumuishaji na uwezeshaji wa wanawake na vijana sambamba na ufungamanishaji wa makundi mengine yaliyotengwa.
MEDA inaamini kuwa moyo/ari ya ujasiriamali na ubunifu unaweza kuwawezesha wajasiriamali wa viwango vyote vya kimapato kuwa kama viongozi wa ukuaji wa biashara unaojali mazingira. MEDA inafanya kazi na biashara, wajasiriamali, na wabia wa ndani ili kukuza uhusika wa biashara katika usimamizi unaofaa wa mazingira na kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi.
MEDA inatumia mbinu inayojumuisha nyanja mbalimbali kwa masuala magumu kuelezeka kimazingira kulingana na mpango wetu. Hii ni pamoja na sera madhubuti iliyowekwa kwa uundaji wa mapato endelevu kimazingira na yanayostahimili tabia nchi, mkakati wa wazi wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi (ECC) na mfumo ambatanishi wa usimamizi wa mazingira (EMS) na vile vile seti ya mbinu na zana zilizoundwa kufikia matokeo yanayofaa kimazingira.
Categories: Resilient Markets Resource Library English 2021 Resources
1621 North Kent Street, Ste 900,
Arlington, VA, 22209
P 202.534.1400
F 703.276.1433
Website Photos: © mari matsuri