Sep 12, 2021 | by MEDA
Katika ulimwengu wetu, watu wa jinsia zote wanaathiriwa na majukumu, matarajio, na tabia zilizowekwa juu yao na jamii. Jinsia, tofauti na jinsi ya kike/kiume, hufunzwa, na inaelezea njia ambazo watu wanaathiriwa na familia zetu, jamii, nchi na dunia. Kupitia shughuli zetu za Usawa wa Kijinsia na Ujumuishaji Jamii (GESI), MEDA inaelewa kuwa wanawake na watu waliotengwa hawaishi peke yao, maisha yao yanaingiliana na ya wengine. Ikiwa mabadiliko yatatokea katika maisha ya mwanamke, kama vile kuongezeka kutegemewa na utambuzi wa haki au kuongezeka kwa ufikiaji fursa, itaathiri wengine katika familia yake. Ili mabadiliko haya yawe na maana na endelevu, lazima wanaume wajumuishwe katika mchakato, ili waelewe sababu na manufaa ya mabadiliko haya na wasitishike na hatua hizi. Vivyo hivyo, wanaume lazima wabadilike ili waweze kutambua mitazamo na tabia zinazodhuru kuhusiana na uanaume na mfumo dume, ambazo hatimaye humwondolea uwezo kila mtu. Lazima pia wachukue hatua ambazo zinafidia ukosefu wa haki wa kihistoria ambao ulinufaisha wanaume kwa njia isiyo ya haki kwa kuwadhulumu wanawake. Kwa mfano, wanawake wanashinikizwa kukaa nyumbani na kuzingatia kuwa walezi na kupuuza maendeleo yao binafsi na ya kiuchumi, wakati wanaume wanaweza kutarajiwa kuhusika katika tabia hatarishi, ukatili, na kukandamiza hisia kwa kupuuza usalama wao binafsi na maendeleo ya kihisia.
Categories: Women's Economic Empowerment Resource Library 2021 Resources
1621 North Kent Street, Ste 900,
Arlington, VA, 22209
P 202.534.1400
F 703.276.1433
Website Photos: © mari matsuri